Shambulizi la kemikali liliwahi kutekelezwa na serikali ya Syriamnamo mwezi Aprili,Kaskazini mwa nchi hiyo.
Marekani ililazimika kujibu shambulizi hilo la kemikali kwa mashambulizi ya kupitia anagani.
Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Ikulu, Sean Spicer, jana Jumatatu ilimuonya rais wa Syria, Bashar Al-Assad, kwamba iwapo serikali yake itatekeleza shambulizi lingine la kemikali, basi yeye na jeshi lake wawe tayari kwa matokeo yatakayokuwa na madhara makubwa.
Hakuna habari zaidi zilizotolewa kuhusu madai hayo ya matayarisho.
Balozi wa marekani kwenye Umoja wa Mataifa, Nikki Haley, aliandika ujumbe kupitia mtandao wa Twitter, kwamba Assad atalaumiwa kwa mashambulizi yoyote mengine dhidi ya raia wa Syria.
Alisema kuwa Russia na Iran, ambazo zimekuwa zikiuunga mkono utawala wa Assad, pia zuitakuwa za kulaumiwa.