Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 07:04

Marekani yaikemea Iran kufanya jaribio la kombora


Balozi Nikki Haley na katibu mkuu wa UN, Antonio Guterres.
Balozi Nikki Haley na katibu mkuu wa UN, Antonio Guterres.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley alisema jumanne kuwa kitendo cha karibuni cha Iran kufanya jaribio la kombora la masafa marefu hakikubaliki kabisa na kwamba utawala wa Trump hautafumbia jicho hatua kama hizo.

Haley alizungumza kwa muda mfupi na waandishi wa habari baada ya kuhudhuria mkutano wake wa kwanza wa kikao cha baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kilichoombwa na Washington. Alisema kwamba wameomba kufanyika mkutano hiyo jumanne ili kuzungumzia kile walichothibitisha kwamba “Iran ilifanya jaribio la kombora la masafa ya kati Januari 29 siku ya jumapili, hilo halikubaliki kabisa”.

Wakati huo huo waziri wa mambo ya nje wa Iran, Mohammed Javad Zarif hakuthibitisha wala kukana chochote juu ya kufyatuliwa kwa kombora hilo. Hata hivyo aliongeza kwamba makombora hayo sio sehemu ya mkataba wa nyuklia. Akiongeza kusema Iran haitatumia kamwe makombora yaliyotengenezwa Iran kushambulia nchi nyingine yeyote.

XS
SM
MD
LG