Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 04:03

Marekani yaendelea kuongoza kwa Medali Rio


London Olympics Cycling Women
London Olympics Cycling Women

Mwendeshaji baiskeli Mmarekani Kristin Armstrong, alishinda dhahabu yake ya tatu mfululizo katika mashindano ya Olimpiki mjini Rio De Jenairo siku ya Jumatano, na kuwa mtu wa kwanza kushinda dhahabu mara tatu mfululizo katika mashindano ya baiskeli ya Olimpiki.

Kwa mujibu wa gazeti la New York Times, Armstrong, ambaye hana uhusiano kiukoo na mwendesha baiskeli mashuhuri Lance Armstrong, alipata medali hiyo siku moja tu kabla ya kusherehekea mwaka wake wa 43 tangu kuzaliwa, na hivyo kuwa mwanamke mzee Zaidi kuwahi kushinda dhahabu katika mashindano ya olimpiki ya kuendesha baiskeli.

Kwa upande wa idadi ya medali zilizonyakuliwa kufikia Jumatano, Marekani na China zilikuwa na dhahabu kumi kila moja, huku Japan, Russia na Uingereza zikifuata kwa kushinda dhahabu sita, nne na tatu mtawalia. Kwa ujumla Marekani inaongoza kwa wingi wa medali, ikiwa na medali thelathini na moja. Ikifuatiwa na China yenye medali 23 huku Japan ikiwa ya tatu kwa kuzoa medali 18.

XS
SM
MD
LG