Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 17, 2025 Local time: 04:41

Marekani yaadhimisha siku ya Mashujaa


Rais Barack Obama akiweka shada la maua kwenye makaburi ya kitaifa ya Arlington, May 26, 2014.
Rais Barack Obama akiweka shada la maua kwenye makaburi ya kitaifa ya Arlington, May 26, 2014.
Wamarekani wanatoa heshima zao kwa wenzao waliofariki wakiwa wanalihudumia jeshi la nchi hii, kwa kuandaa sherehe mbali mbali katika sikukuu ya mashujaa yaani ‘Memorial Day’, inayofanyika kila mwaka siku ya Jumatatu ya mwisho ya mwezi wa Mei.

Rais Barack Obama aliweka shada la maua kwenye kaburi moja la mwanajeshi asiyefahamika katika makaburi ya kitaifa ya Arlington. Jumapili bwana Obama alifanya ziara ambayo haikutangazwa awali huko Afghanistan na kuzungumza na wanajeshi wa Marekani katika kambi kuu la kijeshi mjini Kabul, akisema mafanikio ya kijeshi huko “yamekuja kwa gharama kubwa.”

“Kwenye vituo hapa Afghanistan na miji yote kote Marekani, tutakaa kimya kwa muda mfupi na tutatoa heshima zetu kwa watu wote waliopoteza maisha yao kwa ajili ya uhuru wetu. Na hiyo ni pamoja na takribani wazalendo wa kimarekani 2,200 ambao walipoteza maisha yao, kwa kujitoa mhanga, kwa dhamira ya dhati hapa Afghanistan. Ninafahamu mmesimama mstari wa mbele kwenye mapigano yote. Ninafahamu wengi wenu mna kumbu kumbu za wenzenu waliofariki zikiwa katika mioyo yenu hii leo. Tutawatunuku kila mmoja sio tu kesho lakini daima”.

Sherehe za siku ya mashujaa zinajumuisha gwaride na matukio mengine ya kuwapa heshima mashujaa waliokufa katika miji kote nchini Marekani. Wamarekani wengi hawafanyi kazi na shule zinafungwa hivyo kupelekea wikiendi ndefu ya siku tatu inayochukuliwa kuwa mwanzo usio rasmi wa msimu wa mapumziko, ikiwa ni majira ya joto au summer.

Familia nyingi zinafanya matukio ya kula pamoja kwenye bustani za umaa au kusafiri kuelekea ufukweni au mbuga za kitaifa na viwanja vya kuweka kambi.
XS
SM
MD
LG