Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 10, 2022 Local time: 12:57

Marekani : Wanawake wang'ara tamasha la Tuzo za Grammy za 61


Kutoka kushoto : Maren Morris, Katy Perry, Jimi Westbrook, Kimberly Schlapman, Dolly Parton, Karen Fairchild, Philip Sweet, Miley Cyrus na Kacey Musgraves wakitumbuiza wakati wa tamasha la Grammy ,Jumapili, Feb. 10, 2019, Los Angeles.

Washindi wa kuu wa Tuzo za Grammy za Grammy mwaka 2019 ni wanawake.

Tafrija ya kutoa tuzo hizo ilifanyika kwenye ukumbi wa Staples mjini Los Angeles California, Jumapili.

Tamasha hilo liliongozwa na mwanamuziki mashuhuri Alicia Keys, na limeadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa kampuni ya Motown records iliyowapa jukwa kubwa wanamuziki wenye asili ya kiafrika hapa Marekani.

Washindi wakuu walikuwa muimbaji wimbo wa Country, Kacey Musgraves aliyenyakua Album ya mwaka, na wimbo wake wa Golden Hour, na Childlish Gambino na wimbo wa This is Amerika aliyenyakua rikodi na wimbo bora ya mwaka .

Kacey Musgraves
Kacey Musgraves

Hata hivyo wageni waalikwa, wasanii na watazamaji walifurahishwa pale Alice Kyes alipofungua tamasha akija na magwiji wanawake wa muziki Lady Gaga, Jada Pinkett Smith na Jennifer Lopez lakini pamoja na mgeni ambaye hakutarajiwa hata kidogo Michelle Obama mke wa rais wa zamani Barrack Obama

Tuzo iliyowastajabisha wengi ni ile ya wanamziki chipkizi, aliyonyakua muimbaji muingereza Dua Lipa akiwabwaga .H.E.R na Chole x Halle miongoni mwa wengine kutokana na kibao chake New Rules.

Kati ya wanawake waliong’ara ni Cardi B aliyejipatia Tuzo ya album bora muziki wa rap – Invasion of Privacy na kuwa mwanamke wa kwanza kushinda kwenye kitengo hicho cha Grammy.

Mwanadada chipikizi .H.E.R hakuachwa nyuma kwa kuwa alijipati tuzo ya album bora ya R&B. Ikumbukwe kuwa msanii huyu alijiunga na label ya RCA wakati akiwa mwenye umri wa 14 ingawa sasa anaumri wa miaka 21.

Kandrick Lamar alinyakuwa tuzo ya onyesho bora zaidi kutokana na Kings Dead , huku ile ya wimbo poa zaidi wa rap ikimwendea Aubrey Graham na Daveon Jackson na wimbo wao mwengine Gods Plan.

Kabla ya Tamasha hilo la Jumapili LA Grammy wanamuziki wa Hip Hop mara nyingi hawakupata tuzo za juu ingawa muziki wa rap umekuwa ukiwika katika nyanja muziki hapa Marekani

Ni album mbili tu zawasani wa hip hop walizoweza kupata tuzo ya juu; Lauryn Hills mwaka 1999 ikiwa ni miaka 20 iliyopita na Outkast na wimbo wa Speaker Box the love below 2004.

Basi ni ushindi mkubwa kwa The American kunyakua nafasi hiyo ya juu mwaka huu na Cardi B imeinua hadhi ya wanamuziki wenye asili ya kiafrika. .

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG