Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 11:38

Marekani : Wademokrat wadhibiti mabaraza mawili ya bunge Virginia


Wafuasi wa chama cha Democratic wakiunga mkono chama chao Richmond, Va., Tuesday, Nov. 5, 2019.
Wafuasi wa chama cha Democratic wakiunga mkono chama chao Richmond, Va., Tuesday, Nov. 5, 2019.

Chama cha Democratic cha Marekani kinasheherekea ushindi mkubwa Jumatano kufuatia uchaguzi uliofanyika katika majimbo matatu Jumanne ambapo wamechukua tena udhibiti wa mabaraza mawili ya bunge katika jimbo la Virginia.

Uchaguzi huo wa kawaida katika majimbo hayo ulikuwa pia kipimo cha jinsi uchaguzi mkuu wa 2020 utakavyokuwa pale Rais Donald Trump atakapogombania mhula wake wa pili.

Katika jimbo la kati la Kentucky ambacho hudhibitiwakwa muda mrefu na chamna cha Republican, mgombea wa chama cha Democratic kwa ajili ya kiti cha Gavana Andy Besheer akiwa amepata asilimia 49.2 wakati mpinzani wake wa chama cha Republican Matt Bevin aliyeungwa mkono na Rais Trump hajakubali bado kama ameshindwa.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka 23 ambapo mabaraza mawili ya bunge la Virginia na gavana kudhibitiwa na chama cha Demokratic.

Wachambuzi wanasema inaonekana hili ni wimbi la ushindi wa chama cha Democratic baada ya uchaguzi wa 2018 walipochukuwa udhibiti wa baraza la wawakilishi na pia ni ishara kwamba Warepublican na Rais Trump wanakabiliwa na upinzani mkali uchaguzi wa mwakani.

XS
SM
MD
LG