Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 31, 2024 Local time: 01:12

Marekani yaitaka Sudan Kusini kutii azimio la kusitisha mapigano.


John Kirby msemaji wa wizara ya mambo ya nje.
John Kirby msemaji wa wizara ya mambo ya nje.

Marekani, Umoja wa Ulaya, Uingereza, na nchi zingine majirani wa Sudan Kusini, zimesema kuwa ni sharti serikali ya Sudan Kusini itii azimio la kusitisha mapigano, na kuviita vita vinavyoendelea nchini humo kuwa vya kinyama.

Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Marekani ni ya kwanza kabisa kutaka usitishwaji wa kudumu wa mapigano tangu vita hivyo vilivyoleta maafa kuibuka tena mnamo mwezi Julai mwaka huu katika mji mkuu wa Juba, na kupelekea kutoroka kwa kiongozi wa waasi, Riek Machar, ambaye alitoa wito wa vita vya kujihami.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press, taarifa hiyo ya pamoja ambayo pia iliungwa mkono na mataifa ya Afrika Mashariki, ililaani wito wa Machar wa kutaka mapigano ya kujihami.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilianza nchini Sudan Kusini mnamo mwaka wa 2013, na vurugu hazijasitishwa licha ya makubaliano ya amani ya iliyoafikiwa mwaka mmoja uliopita. Mamia ya watu wamepoteza maisha yao tangu mwezi Julai, huku kwa jumla, maelfu ya raia wakiwa wameuliwa tangu vita hivyo kuanza.

XS
SM
MD
LG