Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:17

Wachambuzi wa Afrika wamulika siasa za Marekani kuelekea Novemba 8


U.S. President Donald Trump and his wife Melania, left, pose for a photo with Britain's Prince Charles and Camilla, the Duchess of Cornwall prior to afternoon tea at Clarence House, in London, June 3, 2019.
U.S. President Donald Trump and his wife Melania, left, pose for a photo with Britain's Prince Charles and Camilla, the Duchess of Cornwall prior to afternoon tea at Clarence House, in London, June 3, 2019.

Wafuatiliaji wa kiafrika wa masuala ya siasa wanazielezea kwa kebehi siasa za Marekani katika yale yaliyobandikwa kwenye mtandao wa Twitter hivi karibuni yakibainisha kuwa uchaguzi wa rais mwaka huu ni sawa na lugha ambayo mara nyingi hutumiwa na waafrika katika uchaguzi.

Mchambuzi wa masuala ya siasa, Ryan Cummings ambaye amechangia mamia ya tweet zake, na ambaye anaendesha taasisi ya ushauri Signal Risk kutoka Cape Town, Afrika Kusini anasema anauona uchaguzi huu ni kituko.

“ Ni kitu ambacho hukitarajii katika sehemu ambako kuna demokrasia kama vile Marekani au pengine kwingine kokote katika dunia iliyoendelea. Mambo yenyewe ni, madai yanayotolewa, na hasa na Donald Trump kuelekea katika upigaji kura.ni jambo ambalo mtu anaweza kulihusisha na wanasiasa wa kiafrika,” anasema Cummings.

Amekataa kumlinganisha Trump, mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican, na mmoja wa viongozi wa kiafrika.

Kwa waafrika wengine katika mtandao wa Twitter wameandika, Trump anafanana na viongozi wa Afrika kwa njia nyingi Zaidi ya moja, hasa pale aliposema kuwa mpinzani wake ni vyema afungwe. Mbinu hiyo ilitumika Ethiopia, Zimbabwe, Zambia na Uganda, kutaja mifano michache tu, baada ya uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali.

Watumiaji wa Twitter wanaeleza kwamba Trump anashutuma za manyanyaso ya ngono kama rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma.

Uwanja wa Twitter barani Afrika umemlinganisha kiongozi wa muda mrefu, kiongozi wa kimabavu wa Gambia na Trump ambaye alijigamba kuhusu ushindi wa kijinsia. Na kama walivyo wanasiasa kadhaa barani Afrika, trump amejitokeza na kudai uchaguzi utagubikwa na wizi dhidi yake.

Kwa upande mwingine, mshindani wa Trump, Hillary Clinton, kama walivyo viongozi wengi wa kiafrika, ni mtu anayetoka katika wasomi wenye nasaba ya kisiasa na uwezo wa kifedha.

Mwandishi wa habari wa International Justice Monitor mjini Nairobi, Tom Maliti anasema wakenya wanatiwa wasi wasi na tTump.

“Kuna hali ya kuicheka Marekani, na inahusu sana ni vipi mfumo wa siasa za Marekani unaweza kuwa na mgombea kama Donald Trump. Na kwa vile hivi sasa ni mgombea, watu wana wasi wasi kwasababu yuko katika nafasi ya kuwa rais wa Marekani, na wanahoji hiyo itakuwa na maana gani,” amehoji Maliti.

Lakini anasema si suala la kucheka. Maliti ameliona hili kwa karibu sana wakati taifa lake lilipokuwa katika hali ya vurugu baada ya uchaguzi wa mwaka 2007, na anasema mataifa mengine yanaiangalia Marekani kama ndiyo mfano.

XS
SM
MD
LG