Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 09:28

Obama, Seneti kupokea taarifa jinsi Russia ilivyoyumbisha uchaguzi Marekani


Rais Barack Obama.
Rais Barack Obama.

Mwenyekiti wa kamati ya shughuli za kijeshi, John Mccain amekiita kitendo cha Russia kuingilia kati uchaguzi ni "kitendo cha kutangaza vita."

Kushukiwa kwa Russia katika kuingilia kati uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2016 itakuwa ni mada itakayo sikilizwa na Seneti ya Marekani Alhamisi, na pia ripoti ambayo atapewa Rais Barack Obama.

Rais ameagiza jumuiya ya wapelelezi kupitia kile kinachofahamika kama uwezekano mkubwa wa uingiliaji kati wa kigeni ambao unarudi nyuma katika uchaguzi wa mwaka 2008 ambao ulimuingiza Obama Ikulu ya White House.

Afisa wa serikali ya Marekani ameithibitishia VOA kwamba Obama atasikiliza matokeo ya uchunguzi huo kuhusu uchaguzi Alhamisi na rais mteule Donald Trump atapewa taarifa hizo pia.

Mashirika ya Upelelezi la Marekani CIA na FBI wamefanya majumuisho kuhusu uchunguzi huo na kukubaliana kuwa serikali ya Russia ilikuwa inahusika na kitendo cha kujipenyeza katika mitandao ya Marekani na kuchota nyaraka kupitia Wikileaks kwa kusudio la kuyumbisha uchaguzi.

Kamati ya Seneti ya shughuli za kijeshi itasikiliza ushahidi kutoka kwa mkurugenzi wa upelelezi wa taifa, James Clapper, mkurugenzi wa shirika la usalama wa taifa, Admiral Michael Rogers, na waziri mdogo wa ulinzi anayehusika na upelelezi Marcel Lettre.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, seneta John McCain Jumatano amekiita kitendo cha Russia kuingilia uchaguzi ni “kitendo cha kutangaza vita.”

“Iwapo unajaribu kuangamiza misingi ya demokrasia, hivyo umeangamiza taifa,” McCain aliwaeleza waandishi wa habari huko Capitol Hill. " Na hivyo basi, kuna namna nyingi za tabaka za vitendo vya kivita. Sisemi kuwa hili lilikuwa shambulio la bomu la atomiki. Kitu ninachoweza kusema unaposhambulia utaratibu wa msingi wa taifa, kitu ambacho wanafanya, hicho ni kitendo cha kivita.”

Kamati ya Seneti ya mambo ya nje itafanya mkutano wake wa faragha ambao utamhusisha afisa wa usalama wa ndani juu ya mitandao Danny Toler na maafisa wa Wizara ya mambo ya nje, Victoria Nuland na Gentry Smith.

XS
SM
MD
LG