Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 08:25

Marekani, Poland, na NATO zakubaliana kuhusu kombora la Ukraine


Katibu mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg akizungumza na wanahabari kuhusiana na kombora la mashariki mwa Poland, akiwa makao makuu ya NATO, Brussels, Novemba 16, 2022.
Katibu mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg akizungumza na wanahabari kuhusiana na kombora la mashariki mwa Poland, akiwa makao makuu ya NATO, Brussels, Novemba 16, 2022.

Maafisa wa Marekani, Poland na NATO, Jumatano wote wamekubaliana kwamba mlipuko uliotokea mashariki mwa Poland na kuuwa watu wawili kuna uwezekano ulisababishwa na kombora la ulinzi wa anga la Ukraine.

Baraza la usalama wa taifa la Marekani limeeleza halijaona chochote ambacho kinapingana na tathimini ya awali ya rais Andrzej Duda kwamba mlipuko kuna uwezekano mkubwa ni wa kombora la ulinzi wa anga la Ukraine ambalo kwa bahati mbaya lilitua Poland.

Lakini Russia imeelezwa kuwa Russia inahusika kwa tukio hilo baya kutokana na uvamizi wake wa miezi tisa nchini Ukraine limesema baraza hilo.

Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin, amewaeleza wanahabari kwamba Ukraine ina kila sababu ya kujilinda yenyewe.

Katibu mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg ametoa tathimini kama hiyo akiwaeleza wanahabari mjini Brussels kwamba si makosa Ukraine ni Russia ambayo iliyosababisha vita ambavyo ni kinyume cha sheria.

XS
SM
MD
LG