Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 00:51

Marekani: Nikki Haley aomba ulinzi kutoka idara ya usalama


Nikki Haley
Nikki Haley

Nikki Haley ambaye anawania uteuzi wa kugombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican ameomba ulinzi kutoka kwa idara ya usalama ya Marekani, kampeni yake imesema Jumatatu.

Haley ni mpinzani pekee aliyebaki dhidi ya rais wa zamani Donald Trump kwa chama cha Republican katika kinyang’anyiro cha mchujo wa GOP - ingawa hawakufichua vitisho vyovyote vilivyowasukuma kutoa ombi hilo. balozi huyo wa zamani katika Umoja wa Mataifa amekuwa akilengwa na matukio mawili ya kuandamwa miezi miwili na taarifa za kupotosha kwa polisi.

Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump

Katika siku za hivi karibuni waandamanaji pia wametatiza kampeni ya Haley huko South Carolina - wakipinga uungaji mkono wake kwa misaada zaidi ya kijeshi kwa Ukraine.

Haley alikuwa Gavana wa Jimbo la South Carolina kuanzia 2011 hadi 2017. Idara ya usalama ya Secret Service mara nyingi hutoa usalama kwa wagombea wakuu wa urais katika chaguzi kuu na za awali.

Hata hivyo, lazima iidhinishwe na Idara ya Usalama wa Taifa, ambao bado hawajatoa maoni kuhusu ombi la ulinzi la Haley.

Forum

XS
SM
MD
LG