Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 17:48

Marekani yaeleza wasi wasi kuhusu Ethiopia kuwashikilia wakaazi wake kwa misingi ya kabila


Mwanamke wa Ethiopia achota kikombe cha ngano baada ya kutolewa na Taasisi ya Huduma za Dharura ya Tigray
Mwanamke wa Ethiopia achota kikombe cha ngano baada ya kutolewa na Taasisi ya Huduma za Dharura ya Tigray

Taarifa hiyo ya pamoja iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje Marekani ilisema Australia, Canada, Denmark, Uholanzi na Uingereza waliungana na Marekani kuitaka serikali ya Ethiopia ikomeshe mara moja kukamatwa kwa watu hao wakisema vitendo hivi vinaongeza ukiukaji wa sheria za kimataifa

Marekani na washirika wake wametoa onyo leo Jumatatu kutokana na ripoti kwamba serikali ya Ethiopia imewashikilia kinyume cha sharia, idadi kubwa ya raia kwa misingi ya kikabila. Taarifa inaeleza kwamba wanasikitishwa sana na ripoti za hivi karibuni za serikali ya Ethiopia, kuwashikilia raia wengi wa Ethiopia kwa misingi ya makabila yao na bila kufunguliwa mashtaka.

Taarifa hiyo ya pamoja iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje Marekani ilisema kuwa Australia, Canada, Denmark, Uholanzi na Uingereza waliungana na Marekani katika kuitaka serikali ya Ethiopia ikomeshe mara moja kukamatwa kwa watu hao, wakisema vitendo hivi vinaongeza ukiukaji wa sharia za kimataifa.

Serikali ya Ethiopia yashutumiwa kwa ukiukaji wa sheria za kimataifa
Serikali ya Ethiopia yashutumiwa kwa ukiukaji wa sheria za kimataifa

Taarifa hiyo ilinukuu ripoti ya tume ya haki za kibinadamu ya Ethiopia (EHCR) na Amnesty International, ambazo zinaelezea kukamatwa kwa watu wa kabila la Tigrayan, ikijumuisha wazee na watoto wadogo. Vita kaskazini mwa Ethiopia vilianza Novemba mwaka 2020, wakati waziri mkuu Abiy Ahmed alipotuma wanajeshi, kuliangusha kundi la Tigray People’s Liberation Front (TPLF), hatua aliyosema ilikuja katika kujibu mashambulizi ya TPLF kwenye makambi ya jeshi la serikali kuu.

XS
SM
MD
LG