Mazoezi hayo yalipima umadhubuti kwa zaidi ya wiki ya joto kali na hali mbaya ya hewa kujiandaa kukabiliana na tishio lolote katika misitu ya tropiki na visiwa vilivyotawanyika majenerali wa Marekani na Ufilipino wamesema.
Utawala wa Rais Biden umekuwa ukiimarisha ushirikiano wa kijeshi katika eneo la Indo-Pacific, ili kukabiliana na China, pamoja na makabiliano yoyote yanayoweza kutokea kwa Taiwan na maeneo mengine ya Asia.
Hatua hiyo imeambatana na juhudi za Ufilipino za kuimarisha ulinzi wa eneo lake huku kukiwa na mizozo inayoongezeka dhidi ya Beijing katika bahari ya South China.
Mazoezi makubwa ya kijeshi ambayo yamefanyika Hawaii, katika miaka ya hivi karibuni chini ya kituo cha pamoja cha utayari wa kimataifa wa Pacific kwa jeshi la Marekani yameanzishwa Ufilipino mwaka huu.
Forum