Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 16:57

Marekani na Kenya zakubaliana kupambana na Ujangilli


Elephant Poaching-Times Square
Elephant Poaching-Times Square
Waziri wa maswala ya ndani katika serikali ya Marekani Bi Sally Jewell, anayezuru Kenya ametia sahihi mkataba wa makubaliano na serikali ya Kenya katika vita dhidi ya uwindaji haramu unaoripotiwa katika mataifa mengi barani Afrika.
Bi Jewell amesema serikali ya Marekani imejitolea kusaidia Kenya sawa na nchi zingine kukabili uovu wa kuangamiza wanyama, katika harakati za kulinda mazingira.
Akiwa katika bandari ya Mombasa waziri Jewell amesema nchi hizo mbili zimekubaliana azimio la kuzuia baishara haramu kama vile dawa za kulevya, pemba za ndovu, na bidhaa haramu zinazopitishwa katika bandari.
Katiza ziara hiyo waziri Sally Jewel aliandamana na balozi wa Marekani nchni Kenya Robert Godec, pamoja na waziri wa mazingira nchini Kenya Bi. Judy Wakhungu.
XS
SM
MD
LG