Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 10, 2022 Local time: 12:26

Marekani na Israel wamefanya majaribio ya makombora ya ulinzi huko Alaska


Kombora aina ya Arrow-3 lililofanyiwa majaribio ya ufanyaji kazi na wote Marekani na Israel huko Alaska

Idara ya ulinzi wa makombora ya Marekani ilieleza kombora aina ya Arrow-3 lina uwezo wa kufika umbali mkubwa. Wakati huo huo Waziri Mkuu wa israel, Benjamin Netanyahu alisema "Maadui zetu wafahamu kwamba tunaweza kukabiliana nao kwa njia zote za ulinzi na mapigano"

Maafisa wa Marekani na Israel walisema majaribio ya mfumo wa pamoja ya makombora ya ulinzi huko Alaska yamefanikiwa. Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu alisema Jumapili majaribio ya makombora aina ya Arrow-3 yanaipa nchi yake uwezo wa kuchukua hatua dhidi ya makombora makali yanayofyatuliwa kutoka Iran na kutoka eneo jingine lolote.

Idara ya ulinzi wa makombora ya Marekani ilieleza kombora aina ya Arrow-3 lina uwezo wa kufika umbali mkubwa. Netanyahu alisema ufanyaji kazi wa makombora hayo ni mzuri. "Maadui zetu wafahamu kwamba tunaweza kukabiliana nao, kwa njia zote za ulinzi na mapigano".

Idara zinazohusika na makombora ya ulinzi ya Marekani na Israel zilipanga kufanya jaribio la kwanza la Arrow-3 kwenye anga ya Alaska kati kati ya mwaka 2018 lakini waliahirisha wakisema kuwa walihitaji kuboresha mfumo huo kuwa tayari kwa shughuli kama hizo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG