Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 09, 2023 Local time: 10:41

Marekani, China zakubaliana kutatua mgogoro wa Korea Kaskazini


Rex Tillerson na Xi Jinping
Rex Tillerson na Xi Jinping

Kwa maneno mzuri yaliotoka kwa Rais wa China Xi Jinping Jumapili, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson amemaliza ziara yake huko Asia tangu achukue madaraka kwa kukubali kushirikiana na China katika kutatua tatizo la Korea Kaskazini.

Wakati huohuo pande zote mbili wakati wa mazungumzo hayo wameyaweka kando mambo yenye utata mkubwa baina ya nchi hizo mbili.

China imechukizwa kwa kuendelea kuambiwa na Marekani izidhibiti silaha za nyuklia za Korea Kaskazini na programu yake ya makombora na pia uamuzi wa Marekani kuweka mfumo wa makombora ya kujihami nchini Korea Kusini.

Beijing pia inatilia mashaka makusudio ya Marekani juu suala la Taiwan kuwa na utawala wake, ambayo China inadai ni sehemu ya nchi yake, wakati uongozi wa Trump ukiandaa seti mpya za silaha kubwa kubwa kwa ajili ya kisiwa hicho kitu ambacho bila shaka kitawakasirisha Wachina.

Kauli za kupongezana

Lakini mkutano uliofanyika katika Ukumbi Mkubwa wa Wananchi huko Beijing, masuala hayo yaliwekwa kando na Xi na Tillerson, angalau mbele ya waandishi, wakati Xi akisema Tillerson amefanya juhudi kubwa kufikia mwanzo mpya mzuri wa mahusiano ya nchi hizi mbili katika kipindi hiki cha mpito.

“Umesema kuwa uhusiano wa China na Marekani siku zote ni wa kirafiki. Napenda kutoa shukurani zangu kwa hili,” amesema XI.

Xi amesema amekuwa akiwasiliana na Rais Donald Trump mara kadhaa kwa simu na ujumbe mfupi.

“Sote tunaamini kuwa ushirikiano wa China na Marekani ndio mwelekeo ambao wote tunafanya juhudi kuufikia. Sote wawili tunategemea mwanzo mpya wa maendeleo ya kujenga mataifa yetu,” Xi amesema.

“Maslahi ya pamoja baina ya China na Marekani yanauzito zaidi kuliko tofauti zetu, na ushirikiano ndio chagua pekee lililosahihi kwa pande zote,” amesema Xi, katika tamko lilotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa China.

China na Marekani zinalazimika kuimarisha ushirikiano katika masuala nyeti ya kimaeneo, kuheshimu maslahi muhimu ya kila upande na mambo muhimu, na kuendelea kulinda mshikamano uliopo kati ya nchi zao, amesema Xi.

Mshirika asiyetabirika

Tillerson ameeleza upande wake kuwa Trump “anathamini kwa hali ya juu mawasiliano ambayo tayari yamefanyika” kati Xi na Trump.

“Na anatazamia kuimarisha uelewano katika fursa ya siku za usoni kwa kutembeleana,” Tillerson amesema.

“Tunajua kuwa kupitia mazungumzo tutaweza kufikia maelewano makubwa ambayo yatapelekea kuimarika na kuimarisha uhusiano kati ya China na Marekani na kuwa na kauli ya makubaliano kwa kuendeleza ushirikiano wetu siku za usoni.”

Mpaka sasa Trump amekuwa hatabiriki kuhusu mtangamano uliopo na China, kwani amekuwa akiishambulia Beijing katika masuala kuanzia biashara mpaka eneo la South China Sea na Disemba kwa kuzungumza na rais wa Taiwan Tsai Ing-wen.

Kabla ya Tillerson kuwasili Beijing Jumamosi, Trump amesema Korea Kaskazini ilikuwa “inatenda uovu” na kuishutumu China kuwa haijafanya juhudi zozote kutatua mgogoro wa program ya silaha ya Korea Kaskazini.

XS
SM
MD
LG