Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Agosti 17, 2022 Local time: 17:32

Marekani na Cambodia zasheherekea miaka 70 ya ushirikiano


Ubalozi wa Marekani Cambodia ukisheherekea miaka 70 ya ushirikiano.

Ifuatayo ni tahariri ya Sauti ya Amerika, inayoelezea sera na msimamo wa serikali ya Marekani.

Mwezi Julai unaadhimisha miaka 70 ya ushirikiano katii ya Marekani na ufalme wa Cambodia.

Tangu Julai 11, 1950 wakati uhusiano wa kidiplomasia ulipoanzishwa kati ya nchi hizo mbili, Marekani na Cambodia zimefanya kazi kwa Pamoja na kuboresha Maisha ya watu wa Cambodia.

Mara nyingine, uhusino kati ya nchi hizo mbili umekuwa usioridhisha kutokana na mizozo ya silaha huko Cambodia.

Hata hivyo, Marekani imeendelea kuwasaidia watu wa Cambodia, ikiwemo kupitia mpango wa ASEAN miaka 1980 ili kufanikisha suluhisho la kisiasa nchini Cambodia ambao matunda yake yalionekana mwaka 1991 kwa kusaini mkataba wa amani mjini Paris.

Wakati serikali ya kifalme iliyochaguliwa kwa njia ya demokrasia ilipoundwa septemba 24 1993, Marekani na ufalme wa Cambodia zilianzisha upya ushirikiano wa kidiplomasia.

Marekani inaendelea kusaidia taasisi za kidemokrasia na kuimarisha haki za kibinadamu nchini Cambodia.

Nchi hizo mbili zinafanya kazi kwa Pamoja kwa lengo la kuimarisha biashara na usalama wa kanda hiyo na dunia kwa jumla.

Marekani inasaendelea kusaidia juhudi za Cambodia kupunguza maambukizi ya virusi vya Ukimwi na magonjwa mengine, kuhakikisha kuwepo lishe bora kwa akina mama na Watoto, kuondoa biashara haramu ya binadamu, ufisadi, kuboresha mazingira, usimamizi bora wa mali asili na kuimarisha ukuaji wa uchumi.

Hii leo, kutokana na janga la virusi vya Corona, Marekani imetoa msaada wa dola milioni 11 kuisaidia sekta ya afya ya Cambodia kukabiliana na janga hilo na kukabiliana na athari za kiuchumi.

Katika mahojiano na Sauti ya Amerika, balozi wa Marekani nchini Cambodia W. Patrick Murphy, amesema kwamba Marekani imewekeza karibu dola bilioni 3 katika muda wa zaidi ya miongo 3, kwa ajili ya kusaidia Cambodia kukabiliana na athari za vita, akiongezea kwamba matokeo mazuri yamepatikana kwenye ushirikiano huo.

Balozi Murphy amsesema kwamba ukuaji wa uchumi umeongezeka na nchi ina utulivu na amani. Juhudi za haki zimechukuliwa kushughulikia madhambi yaliyofanyika siku zilizopita, jambo ambalo ni muhimu sana kwa mfumo wa sheria wakati nchi inaendelea kusonga mbele. Pia, tunaona na kufikiria kuwekeza katika sekta za elimu, afya ya umma, mazingira, sheria na msaada mwingine wa kibinadamu.

Balozi Murphy alisema hivi karibuni kwamba serikali ya Marekani inajitolea kwa dhati kuwasaidia watu wa Cambodia ili kupata maendeleo ya kudumu, kiuchumi na yanayowashirikisha watu wote.

Na hiyo ndiyo tahariri ya Sauti ya Amerika inayoelezea sera na msimamo wa serikali ya Marekani.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG