Carlson alihusika sana katika kampeni ya kuikashifu Dominion, ambayo inatengeneza mashine za kupigia kura, kwamba ilichangia katika wizi wa kura katika uchaguzi wa rais wa 2020.
Carlson mkosoaji mkubwa, alikumbatia itikadi kali za kihafidhina na alikuwa anatoa maoni yake binafsi katika kipindi chake ambacho kilikuwa kinatizamwa na watu wengi.
Kipindi cha “Tucker Carlson Tonight, kilikuwa kikitizamwa na watu wengi sana miongoni mwa Wamarekani walio na umri ulio kati ya miaka 25 na 54.
Baada ya taarifa ya kuachishwa kazi kwa Carlson, hisa za Fox ziliporomoka kwa asilimia 2.9, kampuni hiyo ilitangaza jana Jumatatu.
Dominion ilidai katika kesi yake dhidi ya Fox kwamba Carlson aliruhusu madai yasiyo na msingi kuhusu udanganyifu katika uchaguzi kutololewa katika kipindi chake, huku yeye mwenyewe akionekana kuwa na mashaka kuhusu madai hayo katika jumbe za kibinafsi zilizoonekana katika nyaraka za kesi hiyo.