Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 13, 2024 Local time: 06:26

Marekani kuteuwa balozi mpya kwa Somalia


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani,John Kerry (R) na na Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud. Mei 3, 2014.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani,John Kerry (R) na na Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud. Mei 3, 2014.
Marekani itamteuwa balozi wake wa kwanza nchini Somalia katika muda wa zaidi ya miaka 20.

Waziri mdogo wa masuala ya ndani ya kisiasa, Wendy Sherman alitoa tangazo hilo Jumanne kwenye taasisi ya Marekani inayoshughulika na masuala ya amani. Bibi.Wendy alisema utawala wa Obama umefikia uamuzi wa kumrudisha tena balozi nchini Somalia kulingana na uhusiano wake wa karibu na nchi hiyo na imani yake kwamba wakati mzuri unawadia.

Rais wa Marekani Barack Obama hajasema atamteuwa nani kushika wadhifa huo. Marekani haijakuwa na balozi mjini Mogadishu tangu ilipofunga ofisi zake hapo Januari 5 mwaka 1991.
XS
SM
MD
LG