Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 23, 2023 Local time: 00:41

Marekani kukutana na China wiki hii


Marekani inaandaa uwezekano wa mkutano baina ya waziri wake wa mambo ya nje Antony Blinken, na mwanadiplomasia wa juu  wa China, Wang Yi, wakati wa mkutano wa kikanda wa usalama barani Ulaya Ijumaa hii.

Vyanzo vya kidiplomasia vimeithibitishia VOA kwamba mkutano huo utafanyika pembeni ya mkutano wa kiusalama wa Munich, na unaweza kuwa wa kwanza wa ana kwa ana baina ya wanadiplomasia hao wawili baada ya Marekani kutungua puto la kipelelezi la China mwezi huu.

Tukio hilo lilimfanya waziri Blinken kuahirisha ziara iliyopangwa ya kwenda Beijing.

Waziri Blinken alimweleza Wang Yi kwa njia ya simu Febuari 3 kwamba puto la kipelelezi ambalo lilisukumwa na upepo kuvuka kuingia katika taifa la Marekani, kuwa si kitendo cha kutwajibika, na ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa na dola la Marekani.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG