Vikosi vya Russia vinasonga mbele kuelekea mashariki mwa Ukraine kwa lengo la kuliteka eneo la Donbas ambalo ni kitovu cha viwanda, ambako Ukraine ina hofu kwamba wanajeshi wake watazingirwa na wanajeshi wa Russia.
Katika taarifa, wizara ya ulinzi ya Marekani imesema msaada huo wa thamani ya dola milioni 450 utajumuisha mifumo minne ya ziada ya roketi na mizinga ya masafa marefu, boti 18 za kijeshi za doria kwenye pwani, na maelfu ya silaha nzito zinazofyatua risasi nyingi.
Tangu Russia iivamie Ukraine tarehe 24 mwezi Februari mwaka huu, utawala wa Rais Joe Biden umekwisha toa msaada wa kijeshi wa dola bilioni 6.1 kwa Ukraine.
John Kirby, mratibu kwenye Baraza la usalama wa taifa anayehusika na mawasiliano ya kimkakati, amesema Washington inashirikiana kwa karibu na Kyiv kubaini ni aina gani za silaha zinaweza kukidhi mahitaji yao makubwa katika kila msaada.
“Sababu tunafanya hivi ni kuzingatia kile kinachoendelea kwenye uwanja wa vita,” Kirby amewambia waandishi wa habari kwenye White House.
Facebook Forum