Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 00:54

Marekani kuendeleza ushirikiano na Tanzania


Ziara ya Kaimu Balozi wa Marekani Dkt Inmi Patterson Mwanza nchini Tanzania
Ziara ya Kaimu Balozi wa Marekani Dkt Inmi Patterson Mwanza nchini Tanzania

Serikali ya Marekani imesema kuwa inaona fahari kufanya kazi na Watanzania na kusisitiza inaunga mkono jitihada za wananchi kujenga Tanzania yenye amani, ustawi, usalama na afya.

Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dk Inmi Patterson amesema wakati wa ziara yake mkoani Mwanza Novemba 26 hadi 28, 2017 iliyokuwa na lengo la kukuza uelewa wa wananchi kuhusu jitihada zinazofanywa na Marekani kujenga uwezo wa Watanzania.

Amesema Marekani itaendelea kujenga jamii zenye afya, kukuza uchumi wa jamii na mkoa na kusaidia katika elimu.

Kaimu Balozi aliyasema hayo akiwa katika Shule ya Wauguzi ya Askofu Anthony Mayalla iliyopo katika Hospitali ya Bugando jijini Mwanza.

Wauguzi wa Kimarekani wanafanya kazi na kuwafundisha wenzao wa Kitanzania mbinu za kuwahudumia watoto wachanga na akina mama waliojifungua kama sehemu ya mpango wa ubia wa kutoa huduma za afya duniani.

“Uhusiano wetu mkubwa unaakisiwa na ushirikiano wa kina baina ya nchi zetu na nina imani kuwa, tutaendelea kuimarisha uhusiano huu wa kihistoria tunapoendelea kusaidiana,” alisema.

XS
SM
MD
LG