Akizungumza wakati wa mkutano na waziri mkuu wa Singapore Lee Hsien Loong katika white house, Biden amesema kwamba utulivu wa dunia unakabiliwa na changamoto kadhaa, lakini Washington haijatatizika na vita vya Ukraine.
Biden amesema kwamba anataka kuhakikisha kwamba eneo la Asia pacific ni huru na wazi, hatua ambayo white house inaona kama jaribio la China kutaka kudhibithi eneo hilo kibiashara.
"mipaka haiwezi kubadilishwa kwa lazima, na mataifa yote, makubwa au madogo, yana haki sawa na uhuru, na yana haki ya huo uhuru. Na nataka kukushukuru waziri mkuu na utawala wa Singapore kwa kuunga mkono watu wa Ukraine. Najua kwamba sio rahisi lakini nataka kukushukuru kwa hilo, na umekuwa msitari wa mbele kila wakati umehitajika kufanya hivyo.” Amesema rais Biden
Lee amesisitiza kuhusu ushirikiano mzuri kati ya Marekani na nchi za ASEAN, akisema kwamba utasaidia Marekani kushiriki vikamilifu katika maswala ya Asia-Pacific na kuimarisha zaidi ushirikiano wake na marafiki wengi pamoja na kusimamia maslahi muhimu ya eneo hilo.