Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 11:21

Mvutano kati ya Marekani na Korea Kaskazini juu ya jaribio la kombora unaendelea


Watu wakiangalia kwenye TV pale Korea Kaskazini ilipofanya jaribio la kombora Machi 2016.
Watu wakiangalia kwenye TV pale Korea Kaskazini ilipofanya jaribio la kombora Machi 2016.

Kuna uwezekano mkubwa Marekani kuchukua hatua za kijeshi kutungua kombora hilo kama litafika katika anga za Marekani au washirika wake.

Kuongezeka kwa mvutano kati ya Marekani na Korea Kaskazini kutokana na kuwepo uwezekano wa jaribio la masafa marefu la kombora lenye kichwa cha nyuklia (ICBM), haujaleta mtafaruku wowote huko Asia Mashariki.

Jumapili, Korea Kaskazini ilitangaza kuwa ingefanya jaribio la kombora hilo katika umbali wa anga za kimataifa wakati wowote kutoka sehemu yoyote, kwa mujibu wa msemaji wa mambo ya nje ambaye hakutajwa jina lake, aliyekaririwa na shirika la habari la KCNA.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Ash Carter amejibu hilo jaribio kwa kukiita kitendo hicho cha kurusha silaha ya ICBM “tishio la kweli” kwa Marekani, na amesema kuna uwezekano mkubwa wa kuchukua hatua za kijeshi kulitungua kombora hilo kama litafika katika anga za Marekani au washirika wake.

“Kama ikiwa litaelekezwa kwetu- na kama litakuwa tishio kwetu, ndio tutachukua hatua. Na hivyo ndivyo, ikiwa madhara yake yanakadirika au kuwafikia mmoja wa marafiki zetu au washirika wetu , ndio, tutalitungua,” amesema Carter.

Korea Kusini yasikitishwa na jaribio hilo

Jumatatu, Waziri wa Ulinzi wa Korea Kusini ameiita kauli ya Korea Kaskazini juu ya jaribio la ICBM “ni jambo la kusikitisha” na kueleza kuwa kutakuwa na hatua zitachukuliwa kwa namna ya vikwazo vya kimataifa, lakini haijazungumzia juu ya uwezekano wa Marekani kuchukua hatua za kijeshi.

Iwapo Korea Kaskazini inapuuzia onyo tunalowapa na kuendelea kurusha kombora hilo la ICBM, itakabiliwa na vikwazo vizito na vya nguvu pamoja na shinikizo kutoka Korea Kusini na pia kutoka jumuiya ya kimataifa,” alisema msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Korea Kusini Moon Sang-kyun.

Teknolojia ya ICBM ni ya muda mrefu

Jaribio la la kombora la masafa marefu la ICBM sio kwamba ni teknolojia ambayo haijawahi kutumiwa na Korea Kaskazini. Tayari nchi hiyo imeshafanya majaribio manne ya satalaiti ikitumia silaha zake aina ya Taepodong-2 kama makombora.

Lakini programu ya kaskazini ya angani imelaaniwa vikali duniani kama ni uchokozi katika azma yake ya kutengeneza silaha za nyuklia na teknolojia ya kuzirusha silaha hizo ambazo tayari zimepigwa marufuku na azimio la Umoja wa Mataifa.

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un ameweka wazi mwaka jana hamasa ya serikali yake kufikia nguvu za nyuklia katika kujihami.

Hata hivyo vikwazo vya kimataifa vimeshindwa kuizuia kaskazini kuendeleza kwa nguvu zote juhudi zake kwa kufanya majaribio mawili ya nyuklia na silaha Z4 zinazorushwa na roketi mwaka jana.

XS
SM
MD
LG