Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 09, 2023 Local time: 11:30

Marekani iko pamoja wa Chad katika mapambano dhidi ya Boko Haram


Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Samantha Power akimsikiliza Rais wa Chad, Idriss Debt akijibu maswali ya waandishi wa habari.
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Samantha Power akimsikiliza Rais wa Chad, Idriss Debt akijibu maswali ya waandishi wa habari.

Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, Samantha Power, amesema Marekani inaungana na taifa la Chad na majirani zake katika mapambano yake dhidi ya Boko Haram.

Power yuko katika ziara ya mataifa matatu barani Afrika kuonyesha uungaji mkono wa Marekani wa mapambano dhidi ya kundi la wanamgambo ambalo linafanya harakati zake huko ziwa Chad ambako Nigeria, Chad na Cameroon wanashirikiana mipaka.

Power alizungumza hayo jana Jumatano kwenye mji mkuu wa Chad, N'Djamena kwamba Marekani ianendelea kuunga mkono mapambano dhidi ya kundi la Boko Haram kwa kuwapatia washaurui, taarifa, mafunzo, misaada wa magari na vifaa kwa jeshi la kanda hiyo ili kuweza kupambana na kundi hilo na kuweza kukomboa maeneo zaidi.

XS
SM
MD
LG