Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 01, 2022 Local time: 16:36

Marekani inawashitaki wafanyabiashara wenye uhusiano na Flynn


Michael Flynn, mshauri wa zamani wa usalama wa taifa Marekani

Watu hao wawili walishtakiwa kwenye jimbo la Virginia kwa njama ya kukiuka sheria za Marekani na mmoja kati yao alishutumiwa pia kwa kuwadanganya wachunguzi wa serikali kuu

Marekani inawashitaki wafanya biashara wawili wa zamani wenye uhusiano na aliyewahi kuwa mshauri wa usalama wa taifa kwenye utawala wa Trump, Michael Flynn kwa kuifanyia kampeni ya ushawishi Uturuki kinyume cha sheria ndani ya Marekani.

Bijan Kian, Dec. 17, 2018.
Bijan Kian, Dec. 17, 2018.

Kufunguliwa mashtaka dhidi ya Bijan Kian, m-Marekani mwenye miaka 66 na Ekim Alptekin raia wa Uturuki mwenye miaka 41 kuliwekwa bayana Jumatatu mahakamani kwenye mji wa Alexandria katika jimbo la Virginia nje kidogo na Washington.

Wanaume hao wawili walishtakiwa kwa njama ya kukiuka sheria za Marekani na Apltekin pia alishutumiwa kwa kuwadanganya wachunguzi wa serikali kuu. Marekani iliwashutumu wanaume hao waliofanya kazi na Flynn, ambaye Rais Donald Trump alimtaja kama mkuu wake wa kwanza wa usalama wa taifa mwaka 2017 kabla ya kumfukuza kazi chini ya mwezi mmoja.

Marekani ilisema Kian na Alptekin walikula njama kwa siri kuwashawishi wanasiasa wa Marekani na maoni ya umma dhidi ya kiongozi wa Ki-Islam Fethullah Gulen ambaye Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan anamshutumu kwa kupanga jaribio la mapinduzi lililoshindikana 2016 dhidi ya Uturuki.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG