Uongozi mkuu wa jeshi la Marekani mashariki ya kati (CENTCOM) umemtambulisha afisa huyo mkuu wa Islamic State kama Maher al-Agal, ukimuelezea kama kiongozi wa tawi la IS huko Syria na kama kiungo muhimu kati ya kundi la IS na washirika wake duniani.
“Al-Agal alikuwa na jukumu la kuimarisha maendeleo ya mitandao ya ISIS,” CENTCOM imesema katika taarifa.
Katika taarifa Jumanne, Rais wa Marekani Joe Biden alipongeza shambulio hilo kwa kutuma “ujumbe mkali.”
“Kifo cha Al-Agal kimemuondoa uwanjani gaidi mkubwa na kimepunguza vya kutosha uwezo wa ISIS kupanga, kupata uwezo wa kifedha na kuendesha operesheni katika eneo hilo,” Biden alisema.