Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 09:56

Marekani inasaidia Afrika kuunda mahakama ya uhalifu wa vita


Stephen Rapp, Balozi maalum wa Marekani kwa ajili ya masuala ya uhalifu wa vita

Marekani imeanza mpango wa kusaidia nchi za Afrika na nyenginezo za dunia kuunda mifumo ya mahakama itakayo chunguza na kuhukumu uhalifu wa vita.

Utawala wa rais Barack Obama unania ya kuzisaidia nchi za dunia zilizoa toka katika vita au zinazokabiliwa na ukiukaji mkubwa wa haki za binadam kuunda mahakama thabiti ya kushgulikia uhalifu wa vita.

Kufikia lengo hilo rais Obama amemteua Stephen Rapp mwendesha mashtaka mkuu wa zamani wa mahakama maalum kwa ajili ya Sierra Leone kuwa balozi wake maalum kwa ajili ya masuala hayo.

Akizungumza na Sauti ya Amerika Alhamisi baada ya ziara ya Afrika, balozi Rapp anasema anafanyakazi na baadhi ya nchi za Afrika kuunda mfumo wa mahakama ndani ya nchi hizo ili kuweza kuchuguza na kuhukumu uhalifu wa vita.

“Tunatizana katika baadhi ya nchi za Afrika namna ya kuimarisha mifumo ya mahakama itakayofuatana na kuambatana na misingi ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu. ICC. Mahakama ya The Hague hujiuhusisha pale tu inapodhihirika hakuna nia au uwezo katika kiwango cha kitaifa kuchunguza au kusikiliza na kuhukumu kesi za uhalifu wa vita”.

Moja wapo ya njia za kukabiliana na kesi za uhalifu kama hizo inayopendekezwa katika kiwango cha kitaifa ni kuundwa kwa mahakama ya pamoja, kati ya serikali na raia itakayo hukumu kesi za ukiukaji mbaya sana wa haki za binadam na kupata msaada kutoka kwa watalamu wa kimataifa.

Bw Rapp anasema utawala wa obama unaunga mkono juhudi za ICC kuwahukuwa watu binafsi au makundi yanayotuhumiwa kutenda uhalifu wa vita.

“Kuna kesi nyingi zinazohitaji kusikilizwa, mfano kubakwa kwa wanawake huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kutekwa nyara watoto, na kushambuliwa maelfu ya watu kwa maksudi bila ya kutenda lolote. Kesi hizo zote zinahitaji kushughulikiwa”.

Balozi Rapp anasema anafanya kazi pia pamoja na wizara ya sheria ya Marekani na makundi yasiyo ya kiserikali kuanzisha mahakama ya mchanganyiko huko DRC.

Anasema anafanya kazi pia na maafisa wa Senegal kuunda mahakama ziada kusikiliza kesi ya kiongozi wa zamani wa Chad Hissen Habre, chini ya mamlaka ya Umoja wa Afrika.

Balozi Rapp anasema kwa upoande wa Kenya wametaka kusaidia tangu mapema ili kuunda mahakama maalum ya kusikiliza kesi zinaozhusiana na ghasia baada ya uchaguzi lakini hadi hivi sasa hakuna maendeleo yaliyopatikana pamoja na wakuu wa Kenya.

XS
SM
MD
LG