Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 17:11

Marekani yatakiwa kujihusisha na bara la Afrika


Ed Royce
Ed Royce

Marekani lazima iendelee kujihusisha na maendeleo ya bara la Afrika ambalo kwa sasa linashuhudia baa la njaa na ukosefu wa uthabiti wa kisiasa.

Hayo yamesemwa Alhamisi na mwenyekiti wa kamati ya bunge inayohusika na masuala ya nje, Ed Royce, hivi karibuni Jijini Washington.

Amesema bara la Afrika ambalo linakua haraka kiuchumi duniani likiwa na takriban na wafanyabiashara milioni moja, lina nafasi kubwa ya mahusiano ya kibiashara na Marekani.

Mbunge huyo wa jimbo la California wa chama cha Republikan aliongeza kwamba wakati bara hilo linashuhudia njaa, kuendelea kuwepo na ukosefu wa uthabiti wa kisiasa nchini Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na kwingineko, Marekani lazima iendelee kujihusisha kikamilifu.

Wakati huo huo, Mdemokrat wa cheo cha juu katika kamati ya Royce, mbunge Eliot Engel wa New York amesema kwamba ana wasi wasi kuwa baada ya kujihusisha kikamilifu kwa miaka 16 wakati wa utawala wa George W. Bush na Barack Obama, sera za Marekani kwa bara la Afrika kwa bahati mbaya hivi sasa zimeanza kudidimia.

XS
SM
MD
LG