Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 26, 2024 Local time: 11:49

Marekani ina itaka Misri kuruhusu mikutano ya kisiasa


Ayman Nour (kushoto) mwanasiasa wa upinzani wa Misri akibishana na polisi wa kupambana na ghasia wanaofunga njia mbele ya makao makuu ya chama chake huku mamia ya wafuasi wake wakidai wapewa uhuru zaidi wa kisiasa.
Ayman Nour (kushoto) mwanasiasa wa upinzani wa Misri akibishana na polisi wa kupambana na ghasia wanaofunga njia mbele ya makao makuu ya chama chake huku mamia ya wafuasi wake wakidai wapewa uhuru zaidi wa kisiasa.

Wizara ya mambo ya nchi za nje ya Marekani imesema inabidi Misri iruhusu mikutano ya kisiasa ya amani, uhuru wa vyombo vya habari kuripoti kampeni za uchaguzi, na kuruhusu wafuatiliaji wa kimataifa kabla ya uchaguzi wa bunge unaotazamiwa kufanyika Novemba 28.

Taarifa hii imetolewa kufuatia makundi ya kutetea haki za binadam huko Misri kuonya kwamba kuna msako dhidi ya upinzani.

Hata hivyo Wizara ya mambo ya nchi za nje imeeleza kwamba serikali ya Washington inakaribisha tangazo la serikali ya Misri, kua ina dhamiria kupanua kushiriki kwa makundi zaidi ya kisasa na kuhakikisha uchaguzi wa huru na wa wazi, pamoja na kurahisishia kazi za ufuatiliaji zamakundi ya kiraia nchini humo.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje P.J. Crowley ametoa wito kwa Misiri kuruhusu wafuatiliaji uchaguzi wa kimataifa. Serikali ya Misri imesema itaruhusu makundi ya kiraia ya nchi hiyo kufuatilia uchaguzi wa bunge lakini imekata kuruhusu wafuatiliaji wa kigeni.

XS
SM
MD
LG