Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 16:39

Marekani imetangaza kuunga mkono kuongezwa kwa viti viwili vipya vya kudumu kwa nchi za Afrika kwenye Baraza la Usalama


Linda Thomas-Greenfield, Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, akizungumza baada ya mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Agosti 24, 2023. (AP).
Linda Thomas-Greenfield, Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, akizungumza baada ya mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Agosti 24, 2023. (AP).

Marekani ilitangaza siku ya Alhamisi kwamba itaunga mkono kuongezwa kwa viti viwili vipya vya kudumu kwa nchi za Kiafrika kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lenye nguvu  na kiti cha kwanza kisicho cha kudumu kwa taifa dogo la visiwa linaloendelea.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield alitoa tangazo hilo katika hotuba yake kwa Baraza la Mahusiano ya nje, akiitaja kuwa ni ufuatiliaji wa tangazo la Rais wa Marekani Joe Biden miaka miwili iliyopita kwamba Marekani inaunga mkono kupanua chombo hicho cha wanachama 15.

Wakati Afrika ina viti vitatu visivyo vya kudumu katika Baraza la Usalama, hiyo hairuhusu nchi za Afrika kutoa manufaa kamili ya ujuzi na sauti zao, alisema.

Forum

XS
SM
MD
LG