Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Agosti 14, 2022 Local time: 21:21

Marekani imeshutumu hatua ya rais wa Tunisia kufuta kazi majaji na kuvunja katiba


Rais wa Tunisia Kais Saied

Marekani imemshutumu rais wa Tunisia Kais Saied kwa kile imekitaja kama kukandamiza taasisi za demokrasia nchini humo, baada ya kuwaafuta kazi majaji kadhaa katika hatu ainayoonekana kama ya kujilimbikizia mamlaka zaidi.

Saied, ambaye pia ameivunja tume ya uchaguzi na kusema kwamba atabadilisha katiba mwezi huu, amewashutumu majaji kwa ufisadi na kuwalinda magaidi.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Ned Price, amesema kwamba hatua ya Saied kufuta kazi majaji ni sehemu ya hatua za kutisha ambazo amechukua kuvuruga taasisi huru za kulinda demokrasia ya Tunisia.

Katika kikao na waandishi wa habari, Price amesema kwamba maafisa wa Marekani walikuwa wamewasiliana na wenzao wa Tunisia kuhusu umuhimu wa kuwepo taasisi huru zenye uwezo wa kusimamia demokrasia.

Amesema kwamba Marekani inaendelea kuitaka Tunisia kuhakikisha kwamba kuna mchakato huru unaokuza demokrasia.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG