Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 12:57

Marekani yafanya shambulizi dhidi ya Al Shabaab Somalia


Wanamgambo wa kundi la al Shabaab la nchini Somalia.
Wanamgambo wa kundi la al Shabaab la nchini Somalia.

Marekani imesema imefanya mashambulizi ya kujilinda ya anga kwa wapiganaji wa kundi la al-Shabaab nchini Somalia na kuwauwa wanamgambo wasiopungua tisa.

Pentagon ilitangaza shambulizi hilo la anga siku ya Jumatano na ripoti pia zilithibitishwa na serikali ya Somalia. Lakini maafisa wa Somalia walisema shambulizi la Marekani kati kati ya mji wa Galkayo liliuwa wanajeshi wake 22 na kuwajeruhi 16 wengine.

Hata hivyo Pentagon ilipoulizwa juu ya ripoti ya serikali ya Somalia, ofisa mmoja wa Marekani alisema “hatudhani kama shutuma hizi zina ukweli wowote”.

Waziri wa usalama wa kikanda wa Somalia, Osman Isse Nur, aliiambia Sauti ya Amerika-VOA kwamba shambulizi lililenga kituo kimoja nje ya kijiji cha Jehdin, kilomita 30 mashariki ya Galkayo.

Bwana Nur alilaumu vikosi vya kijasusi katika utawala wa jimbo jirani la Puntiland kwa kutoa taarifa zisizo sahihi kwa Marekani.

XS
SM
MD
LG