Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 20, 2025 Local time: 15:57

Marekani haijapata uthibitisho wa vyombo ilivyotungua ni vya ujasusi


Serikali ya Marekani, Jumanne imesema kwamba mpaka sasa haina uthibitisho kwamba vyombo vinne vilivyotunguliwa angani wiki iliyopita katika anga la Amerika kaskazini vilikuwa na uhusiano na China ama programu yoyote ya ujasusi ya taifa la nje.

Wapelelezi wa Marekani mpaka sasa hawaja ona ishara yoyote ama kitu chochote kinacho onyesha mahsusi wazo kwamba vyombo hivyo vitatu vilikuwa ni sehemu ya ujasusi wa China, ama juhudi zozote za ujasusi alisema msemaji wa baraza la usalama wa taifa la Marekani, John Kirby.

China imeendelea kudai kwamba puto lililokosea njia lilikuwa likikusanya taarifa za hali ya hewa na kusukumwa na upepo mpaka kuvuka Marekani kimakosa.

Lakini maafisa wa Marekani wanasema wamepata vipande vyake na kuhitimusha kwamba lilikuwa katika uchunguzi wa hali ya juu katika kambi za jeshi la Marekani.

XS
SM
MD
LG