Serekali imesema haiamini kwamba vyombo hivyo vilikuwa ni vya uchunguzi licha ya kwamba inaacha wazi uwezekano kuwa vilikuwa vinafanya jambo hilo.
Msemaji wa Baraza la Usalama wa Taifa, John Kirby, aliwaeleza wanahabari akiwa White House kwamba vyombo hivyo vilikuwa haviendeshwi na havikuwa na uwezo wa kufanya upelelezi licha ya kwambaa uwezekano huo wanauchunguza.
Amesema sehemu za vyombo hivyo vilidondokea maeneo ya mbali ambayo ni vigumu kufikika. Vilidondokea Marekani na Canada, na wanajeshi wa mataifa hayo mawili wanajaribu kutafuta vipande hivyo, ambavyo Kirby alikataa kutaja kama ni maputo.
Facebook Forum