Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 11:25

Gbagbo apewa siku kadhaa kujiuzulu

Polisi wa Ivory Coast wanaomtii Rais Laurent Gbagbo wakikabiliana na wafuasi wa Alassane Ouattara
Polisi wa Ivory Coast wanaomtii Rais Laurent Gbagbo wakikabiliana na wafuasi wa Alassane Ouattara

Marekani inasema jumuiya ya kimataifa inamuonya rais asiyetambulika wa Ivory Coast Laurent Gbagbo, kwamba anasiku kadhaa za kujiuzulu au kukabiliana na vikwazo.

Marekani inasema jumuiya ya kimataifa inamuonya rais asiyetambulika wa Ivory Coast Laurent Gbagbo, kwamba anasiku kadhaa za kujiuzulu au kukabiliana na vikwazo.

Afisa mmoja mwandamizi wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani alisema jana kwamba Marekani, Ufaransa na nchi za Afrika zimempa bwana Gbagbo muda wa kujiandaa kukabidhi nchi ndani ya kile alichokiita muda maalum. Aliongeza kwamba bwana Gbagbo inaonekana anaielewa hali ilivyo.

Onyo kutoka Washington lilifuatia mapigano mapya Alhamisi kati ya wanajeshi wanaomuunga mkono Gbagbo na waasi wa zamani wanaomuunga mkono mpinzani wake, Alassane Ouattara.

Mapigano yalizuka katika mji mkuu Abidjan na mji wa kati wa Tiebissou, ambao upo katika mstari unaoligawa eneo kati ya kaskazini linalodhibitiwa na waasi na kusini inayotawaliwa na serikali. Msemaji wa bwana Gbagbo alisema watu 20 waliuwawa katika mapigano huku wafuasi wa bwana Ouattara walisema idadi ya vifo ni watu wasiopungua 30.

XS
SM
MD
LG