Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 23:31

Marekani yafunga Ubalozi wake Gambia


Adama Barrow akiapishwa kwenye ubalozi wa Gambia nchini Senegali.
Adama Barrow akiapishwa kwenye ubalozi wa Gambia nchini Senegali.

Wakati huo huo kiongozi wa siku nyingi nchini humo, Yahya Jammeh amenangania madarakani akikaidi kumpisha rais mteule mpya Adama Barrow.

Barrow, aliyeshinda uchaguzi mwezi uliopita, ameapishwa rasmi Alhamisi katika nchi ya jirani ya Senegal.

Rais Jammeh anaendelea kunang’ania madaraka katika mji mkuu Banjul akidai kuwa kulikuwa na mapungufu katika uchaguzi, ingawaje hapo awali alikubali matokeo.

Baraza la Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kauli moja lilipitisha azimio linalomtaka Jammeh kuachia madaraka.

Majeshi ya mataifa jirani na Gambia yamekusanyika katika mpaka wa Gambia kumsaidia Barrow kuchukua nafasi yake ya ushindi iwapo atahitaji msaada.

Mwandishi wa VOA, Zlatica Hoke amesema ushindi wa Barrow wa Disemba 1 katika uchaguzi ni ishara ya kumalizika kwa utawala wa Jammeh uliodumu kwa zaidi ya miaka 20.

Baada ya kushindikana kuapishwa katika nchi yake, rais mteule aliapishwa Alhamisi katika ubalozi wa Gambia nchini Senegal.

Rais wa Gambia Barrow amesema: “Udumu umoja wa watu wa Gambia. Kwenda mbele daima na hakuna kurudi nyuma. Ahsanteni sana.”

Huko nyumbani wafuasi wa Barrow wamekuwa wakisheherekea kuapishwa kwake kwani hawakuweza kuhudhuria.

Mfuasi wa Barrow, Lamin Jao amesema: Dikteta hayuko tena. Kila wakati alikuwa anawakandamiza watu.”

Mfuasi huyo aliongeza: “Ni suala la muda. Ni karibuni hivi tutamuondoa kabisa, amini hilo.”

Wafuasi wa Adama Barrow wakisheherekea kuapishwa kwake nchini Gambia
Wafuasi wa Adama Barrow wakisheherekea kuapishwa kwake nchini Gambia

Mwandishi wa VOA anaendelea kusema kuwa mara ya kwanza Jammeh alikubali kushindwa, lakini baadaye alidai kuwa uchaguzi ulichakachuliwa kwa msaada uliotoka nje, na akakataa kuachia madaraka.

Barrow aomba msaada Umoja wa Mataifa

Kwa mujibu wa VOA Barrow ameomba msaada kutoka Umoja wa Mataifa na nchi zilizo jirani na Gambia za Afrika Magharibi.

Katika hatua nyingine Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Alhamisi lilipitisha azimio kuthibitisha ushindi wake na msaada aliyouomba .

Naibu Balozi wa Uiingereza katika Umoja wa Mataifa, Peter Wilson amesema:

Azimio hilo liko wazi: Rais wa zamani Jammeh lazima aheshimu uamuzi wa wananchi wa Gambia na kukabidhi madaraka mara moja.”

Majeshi ya Senegal

Majeshi ya Senegal yameingia Gambia muda mfupi baada ya Baraza la Usalama kupiga kura Alhamisi kuidhinisha kuondolewa kwa Jammeh kwa nguvu kama ikibidi. Nchi nyingine za Afrika Magharibi pia zinapeleka majeshi. Barrow hata hivyo amewaonya wanajeshi wa nchi hiyo wasijaribu kukaidi.

Rais huyo amesema: “ Naamuru wanajeshi wote wabakie katika kambi zao. Wale ambao watakutwa wakikaidi au wamebeba silaha bila ya kibali watahesabiwa ni wapinzani.”

Mwandishi wa VOA amesema kuwa Marekani inawafiki hatua za kijeshi zilizochukuliwa na nchi za Afrika Magharibi ambazo ni jirani na Gambia katika kusaidia kumweka madarakani rais huyo mpya.

Marekani yatahadharisha raia wake

Msemaji wa wizara ya Mambo ya Nje ya Marekan, John Kirby amewatahadharisha raia wamarekani walioko nchini Gambia juu ya uwezekano wa kuwepo kwa ghasia.

“Tayari tumewajulisha raia wa Marekani kwenda katika eneo lenye usalama kutokana na hatari za kuzuka mapigano. Na kwa uangalifu mkubwa, tumewataka wawe wanatathmini hali ya usalama wao kabla ya kurudi kufanya shughuli zao. Pia wameshauriwa ikiwezekana kuondoka nchini Gambia,” amesema msemaji Kirby.;

XS
SM
MD
LG