Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 13, 2024 Local time: 11:56

Bado ipo migongano katika Bunge la Marekani


Spika wa Baraza la Wawakilishi, Paul Ryan.
Spika wa Baraza la Wawakilishi, Paul Ryan.

malumbano yaliyojitokeza yameleta picha isiyo ya kawaida kwa kiwango cha juu: ikiw akiongozi wa serikali inayomaliza muda wake na washawishi wakuu katika bunge kwa utawala unaoingia madarakani wakiwa wamehitilafiana kabisa.

Katika migongano inayoendelea na itayokuja katika uongozi, imemlazimu rais Barack Obama kwenda kwenye bungeni Jumatano ikiwa ni katika juhudi za kuilinda sheria ya Afya aliyoipitisha katika kipindi chake cha urais.

Wakati huo huo makamu rais mteule, Mike Pence alifika bungeni ili kujenga msimamo wa chama chake cha Republikan ambao umekusudia kuifuta kumbukumbu ya Obama ya afya pale Donald Trump atapochukua urais mapema mwezi huu.

Malumbano hayo yamejitokeza yakibainisha picha isiyo ya kawaida kwa kiwango cha juu: ikiwa kiongozi wa serikali inayomaliza muda wake na washawishi wakuu katika bunge kwa utawala unaoingia madarakani wakiwa wamehitilafiana kabisa.

Wabunge na maseneta wa Chama cha Demokratik wakiwa bado wanajiuguza kutokana na matokeo ya uchaguzi wa mwaka jana, walifika kwenye mkutano wa faragha na rais wakisema walikuwa wametiwa moyo na kuazimia kupigania mambo ya msingi na itikadi hata baada ya Obama kuondoka, kiongozi ambaye ni mwenzao anayeondoka madarakani Januari 20.

“ Obama alikuwa ni mtu mwenye kuhamasisha,” amesema seneta wa walio wachache, Chuck Schumer wa New York. “ Tuna matumaini makubwa kwamba mambo mazuri ambayo yamefanyika katika sheria ya Affordable Care yataendelea kuwepo.”

Hata hivyo siku ya kwanza ya bunge jipya la Marekani Jumanne kulikuwa na malumbano makali wakati warepublikani katika bunge lililokuwa na wawakilishi wengi zaidi walipofanya njama kubadilisha kanuni zinazoiongoza kamati ya maadili, lakini ghafla wakafuta mpango huo kufuatia malalamiko katika bunge na kukemewa na rais mteule, Donald Trump.

Warepublikani walijiandaa kuchukua madaraka ya bunge kwa kuiteka nyara ofisi iliyokuwa inajitegemea bila ya mafungamano ya kisiasa, hatua ambayo ingeizuia kamati hiyo kuwachunguza wawakilishi ambao wanashukiwa kukiuka maadili au kujihusisha na jinai.

Katika tamko lililokuwa linakazania mabadiliko, spika wa bunge, Paul Ryan alisema kamati hiyo ya maadili inahitaji kufanyiwa mabadiliko “lakini akang'ang'ania” kuwa itaendelea kufanya shughuli zake bila ya kuingiliwa na kuhakikisha kwamba kuna uwajibikaji katika bunge.

Saa chache baadaye, spika na wafuasi wa Republikan bungeni walibadilisha msimamo wao wakati kelele za kupinga uamuzi huo zilipotinga kutoka pande zote mbili za bunge.

“Hili ni jambo linatatiza sana na ni dalili mbaya ya matokeo yanayokuja, “seneta mpya aliyeapishwa, Chris Van Hollen aliiambia VOA.

XS
SM
MD
LG