Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 15, 2026 Local time: 18:58

Marekani: Biden na MacCarthy wamefikia makubaliano ya kifedha

Rais wa Marekani Joe Biden (Kulia) akiwa na spika wa baraza la wawakilishi Kevin McCarthy katika White House, Washington
Rais wa Marekani Joe Biden (Kulia) akiwa na spika wa baraza la wawakilishi Kevin McCarthy katika White House, Washington

Rais wa Marekani Joe Biden amefikia makubaliano na spika wa baraza la wawakilishi Kevin McCarthy kuhusu mswaada wa kuongeza uwezo wa Marekani kukopa pesa zaidi na kuepuka uwezekano wa kushindwa kulipa madeni yake.

Wahusika katika mazungumzo hayo sasa wanaharakisha kumalizia kuuandika mswaada huo.

McCarthy amesema kwamba baraza la wawakilishi litapiga kura Jumatano kufanya uamuzi wa mswaada huo na kutoa fursa kwa baraza la senate kuupitisha kabla ya Juni 5 ili kuhakikisha kwamba Marekani haishindwi kulipa madeni yake.

Hata hivyo mambo mengi yaliyomo kwenye mswaada hayajulikani kwa umma japo pande zote katika bunge zinatarajia kutangaza ushindi wao.

Makubaliano hayo yataiwezesha Marekani kuongeza kiwango chake cha kukopa kwa muda wa miaka miwili ijayo.

This item is part of

Forum

XS
SM
MD
LG