Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 19, 2024 Local time: 16:50

Marekani: Afisa wa zamani wa polisi Chauvin akata rufaa


Derek Chauvin.
Derek Chauvin.

Afisa Polisi wa zamani wa mji wa Minneapolis, jimbo la Minnesota, Marekani, Derek Chauvin, Alhamiasi alikata rufaa dhidi ya hukumu aliyopewa kwa mauaji ya mwanaume Mmarekani mweusi George Floyd,

Chauvin, mwenye umri wa maiak 46 aliwasilisha malalamishi 14 yanayohusiana na kesi yhiyo iliyosikilizwa mapema mwaka huu.

Kifo cha Floyd, mwenye umri wa miaka 46, kilichotokea mwezi Mei mwaka jana, kilisababisha maandamano makubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini Marekani, na sehemu zingine duniani, kwa miongo kadhaa, ya kupinga ubaguzi wa rangi.

Chauvin, ambaye mwezi Juni mwaka alihukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka 22 gerezani kwa kumuua Floyd kwa kupiga magoti shingoni kwa karibu dakika 10, alikata rufaa juu ya hukumu hiyo Alhamisi usiku mbele ya mahakama ya wilaya ya Minnesota, siku ya mwisho, ambayo aliruhusiwa kufanya hivyo, kwa mujibu wa sheria.

Katika hoja zake, analalamikia hali ya "utovu wa nidhamu wa kibaguzi" na anaorodhesha masuala kadhaa kuhusu jopo lililochaguliwa kusikiliza kesi hiyo, kati ya pingamizi zingine.

XS
SM
MD
LG