Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 01, 2023 Local time: 15:09

Marais wa Sudan kaskazini na kusini kufanya mazungumzo muhimu kuhusu Abyei


Walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa - UNMIS - walipokuwa wakifanya doria huko Abyei, Sudan Kusini mapema mwezi Machi mwaka huu.

Rais wa zamani wa Afrika Kusini kuwakutanisha Rais Omar al-bashir na Rais Salva Kiir.

Marais wa Sudan kaskazini na kusini wanapanga kukutana Jumapili, huku mapigano yakiendelea kupambana moto kwenye mpaka wa kaskazini na kusini.

Kiongozi wa kaskazini Omar al-Bashir na kiongozi wa kusini Salva Kiir watakuwa na mazungumzo muhimu katika mji mkuu wa Ethiopia, mazungumzo ambayo yanasimamiwa na rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki.

Umoja wa Afrika, ambayo ni mwenyeji wa mkutano imsema viongozi hao watajadili kuondolewa kwa wanajeshi kutoka kwenye mkoa wenye mzozo wa Abyei na uwezekano wa kupelekwa kwa walinzi wa amani wa kiafrika.

Majeshi ya kaskazini mwezi uliopita yamekamata udhibiti wa mkoa wenye utajiri wa mafuta wa Abyei, na kuchochea maelfu ya wakazi kulikimbia eneo hilo.

Katika tukio tofauti, majeshi ya kaskazini yamekuwa yakipigana na makundi yenye silaha katika jimbo la mpakani la Kordofan Kusini kwa zaidi ya wiki moja. Jeshi la kaskazini limekanusha ripoti kwamba ndege zake mbili za kivita zimeangushwa huko Kordofan Kusini.

Sudan Kusini imepanga kujitangazia uhuru wake katika kipindi cha chini ya mwezi mmoja, baada ya kupiga kura kutaka kujitenga na kaskazini wakati wa kura ya maoni ya Januari.

Kaskazini na kusini awali walipigana vita vilivyodumu kwa takriban miaka 21, vita hivyo vilimalizika mwaka 200. Ghasia katika mkoa wa Abyei na Kordofan Kusini zimeongeza wasi wasi kuwa Sudan huenda ikatumbukia tena kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.

XS
SM
MD
LG