Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 11:30

Maprofesa na wahadhiri wanatishia kufanya mgomo Sudan Kusini


Mwanafunzi akiangalia kwa makini ramani ya Sudan Kusini
Mwanafunzi akiangalia kwa makini ramani ya Sudan Kusini

Maprofesa na wahadhiri kutoka vyuo vikuu vitano nchini Sudan Kusini wametishia kuitisha mgomo Jumatano kama serikali haitawalipa mishahara yao ya nyuma ya takriban miezi mitatu na mafao mengine kwa mwaka mzima uliopita.

Waziri mdogo wa elimu ya juu nchini Sudan Kusini alisema wizara yake inafahamu madai ya wafanyakazi wa vyuo vikuu, lakini serikali haina njia ya kupata fedha hizo.

Wawakilishi kutoka vyuo vikuu vitano vya umma huko Sudan Kusini waliitisha mkutano wa waandishi wa habari mjini Juba siku ya Jumanne kutangaza mgomo wao.

Philip finish Apollo, msemaji wa umoja wa wafanyakazi wa vyuo vikuu na kaimu rais wa chama cha wafanyakazi katika chuo kikuu cha Juba alisema maprofesa na wahadhiri wameapa kuitisha mgomo mei 25 na kubaki nyumani mpaka wizara ya fedha itakaposuluhisha madeni yao yote ya zamani na kuwapatia marekebisho ya mishahara mipya.

Vyuo vikuu vitano vya umma ni pamoja na chuo kikuu cha Juba, Upper Nile, Bahr el Ghazal, Rumbek na chuo kikuu cha kumbukumbu ya Dr. John Garang cha sayansi na teknolojia.

Apollo alisema mishahara ambayo wahadhiri wanadai inafikia paundi milioni 28 kwa fedha za Sudan Kusini sawa na dola milioni 4.6. Apollo Alisema mgomo utawaathiri wanafunzi.“ufundishaji kwa hakika utaathirika, hakuna atakayekwenda darasani, mambo ambayo yanahusiana na kufanya utafiti, kuwafuatilia wanafunzi; kwa hakika hizi zote ni shughuli ambazo wafanyakazi wa chuo kikuu wanazifanya na kwa hakika yote haya yatasitishwa”.

Mpaka serikali itakapojibu madai ya wafanyakazi wa chuo kikuu katika muda wa saa 24, Apollo alisema mgomo utaendelea kama ulivyopangwa.

Profesa Bol Deng, waziri mdogo wa elimu ya juu alisema wizara yake imefanya kila iwezalo kuzungumzia madai hayo. Alisema maafisa wa wizara ya elimu wamewasilisha madai hayo kwenye wizara ya fedha, ambayo ni taasisi ya serikali inayohusika na malipo.

XS
SM
MD
LG