Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 29, 2023 Local time: 05:38

Mapigano Yemen kusitishwa


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry amesema sitisho la mapigano nchini Yemen linaweza kuanza kutekelezwa Novemba 17, ikiwa kila mtu atatenda wajibu wake.

Vuguvugu la Wahouthi wa Yemen wenye silaha na ushirika wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia umekubaliana kuunga mkono suluhisho la mgogoro nchini Yemen.

Hiyo yote ni kulingana na muundo uliowekwa kwa kuunda serikali mpya ya Yemen ya umoja wa kitaifa ifikapo mwisho wa mwaka huu.

Mpango wa Oman, ambao ulifanikishwa na juhudi za Bwana Kerry, unatoa mwito kwa rais wa Yemen, Abdu Rabu Mansour Hadi kukabidhi madaraka kwa naibu wake ili Wahouthi waweze kuondoka kutoka katika miji mikuu ya Yemen.

XS
SM
MD
LG