Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 03:58

Mapigano yazuka katika mji mkuu wa Libya


Magari yaliyoharibiwa baada ya mapigano kati ya wanajeshi watiifu kwa mkuu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya, Abdulhamid al-Dbeibah na vikosi pinzani yanaonekana Tripoli, Libya, Mei 17, 2022. Tripoli, Libya, May 17, 2022. REUTERS/Hazem Ahmed
Magari yaliyoharibiwa baada ya mapigano kati ya wanajeshi watiifu kwa mkuu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya, Abdulhamid al-Dbeibah na vikosi pinzani yanaonekana Tripoli, Libya, Mei 17, 2022. Tripoli, Libya, May 17, 2022. REUTERS/Hazem Ahmed

Mapigano makali yamezuka katika mji mkuu wa Libya, Tripoli  wakati wa usiku baada ya moja ya makundi hasimu  kupambana vikali na milio mikubwa risasi ilisikika kote mjini humo.  

Mapigano hayo yametokea katikati mwa mji wa Tripoli, mashahidi walisema, bada ya moja ya makundi yenye nguvu kushambulia ngome ya hasimu wake na kupelekea saa kadhaa za ufyatuaji wa risasi ya na kusababisha khofu kusambaa kote mjini humo.

Serikali ya Umoja wa Kitaifa yenye makao yake makuu mjini Tripoli (GNU) na utawala hasimu unaoungwa mkono na bunge lenye makao yake mashariki mwa nchi walitupiana lawama kuhusu mapigano hayo, huku khofu ikiongezeka miongoni mwa Walibya wengi kuhusu mzozo mkubwa zaidi kuhusu mzozo wa kisiasa wa Libya.

Mapigano yoyote kati ya makundi yenye nguvu ya Tripoli yana hatari ya kujitokeza katika makundi mengine, na mapigano ya Jumamosi yamedumu kwa muda mrefu kuliko ghasia nyinginezo katika mji huo kwa miezi kadhaa.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya ulielezea wasiwasi wake kuhusu mapigano hayo, ikiwemo kile walichokiita mashambulio ya wastani na makali katika vitongoji vinavyokaliwa na raia.

XS
SM
MD
LG