Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 20:18

Mapigano yaendelea Bamako


Kaimu rais wa Mali Dioncounda Traore
Kaimu rais wa Mali Dioncounda Traore

Wanajeshi watiifu kwa rais aliyepinduliwa wapigana na waasi

Mapigano ya bunduki yalizuka mapema Jumannne katika mji wa Bamako nchini Mali, siku ya pili ya mapigano makali baina ya wanajeshi waasi na wale watiifu kwa rais aliyepinduliwa madarakani Amadou Toumani Toure. Walioshuhudia walisema milio ya risasi ilisikika nje ya kituo cha utangazaji cha kitaifa na kwenye kituo cha kijeshi cha Kati, makao makuu ya wanajeshi waasi. Wanajeshi hao waasi walisema katika taarifa kupitia televisheni Jumanne kuwa wanadhibiti maeneo muhimu ya mji mkuu. Walisema shambulizi dhidi yao limefanywa na watu wenye nia mbaya ambao lengo lao ni kuyumbisha mchakato wa makabidhiano ya madaraka kikatiba. Mapigano ya Jumatatu yalifuatia jaribio la kumkamata mlinzi wa rais Toure ambaye pia alikuwa mwanajeshi wa ngazi ya juu. Wanajeshi waasi walipindua serikali mwezi Machi na kumshtumu rais huyo kwa kushindwa kuwapa vifaa kuwawezesha kulidhibiti kundi la waasi wa Touareg kutoka kaskazini mwa nchi.

XS
SM
MD
LG