Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 25, 2024 Local time: 21:22

Mapigano makali yaripotiwa Soledar


Wanajeshi wa Ukraine wanaotumia silaha ya Howitzer Panzerhaubitze 2000, ya Ujerumani karibu na Soleda. REUTERS
Wanajeshi wa Ukraine wanaotumia silaha ya Howitzer Panzerhaubitze 2000, ya Ujerumani karibu na Soleda. REUTERS

Naibu Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Hanna Malyar alisema Alhamisi kulikuwa na mapigano makali huko Soledar, lakini  vikosi vya Ukraine vinaendelea kupambana.

Malyar alizungumza siku moja baada ya madai yanayokinzana kuhusu ni nani anayedhibiti mji huo wa mashariki mwa Ukraine.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin siku ya Jumatano aliita vita vya Soledar mazingira yenye kubadilika sana, vita vikali huku kukiwa na ripoti kwamba mji ulikuwa umeanguka kwa Warussia.

Kwa wakati huu, hatuwezi kuthibitisha taarifa hiyo, Austin alisema katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na waziri wa mambo ya nje Antony Blinken na wenzao wa Japan katika wizara ya mambo ya nje.

XS
SM
MD
LG