Kundi la M23, ambalo wapiganaji wake wanatokea kabila la Watutsi, limekuwa likidhibiti sehemu kadhaa za Kivu kaskazini.
Kundi hilo limetoa taarifa Jumamosi, likilishutumu jeshi la DRC kwa kushambulia ngome zake kwa mabomu, na kuuawa raia 15 wakiwemo Watoto wawili, madai ambayo hajayathibitishwa.
Mapigano hayo yanajiri siku moja baada ya jeshi la Kenya kuingia DRC chini ya makubaliano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, kuisaidia nchi hiyo kupambana na makundi ya waasi.
Uhusiano kati ya DRC na Rwanda umeharibika kufuatia mashambulizi ya kundi la M23, DRC ikisisitiza kwamba waasi hao wanaungwa mkono na Rwanda. Ripoti ya Umoja wa Mataifa ambayo haijawekwa wazi, inasema kwamba Rwanda inawaunga mkono waasi hao.
Rais mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta anatarajiwa mjini Kinshasa leo Jumapili kuendelea na mchakato wa amani nchini DRC. Ziara yake inajiri siku moja baada ya rais wa Angola Joao Lourenco kukutana na rais Felix Tshisekedi wa DRC, baada ya kutembelea Rwanda ijumaa.