Waasi walishambulia kambi za jeshi la Congo za Nyesisi kilometa 35 kaskazini mwa Mji wa Goma karibu na mbuga ya wanyamapori ya Virunga.
Eneo hilo lililokuwa na mashambulizi sehemu moja ipo upande wa DRC na sehemu nyingine upande wa Rwanda.
Kanali Ndjike Gylaume msemaji wa jeshi la FARDC Kivu kaskazini ameiambia Sauti ya America kwamba jeshi la Congo linapambana vikali na waasi hao likitumia silaha nzito.