Pendekeo la Umoja wa Ulaya la kufufua makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015 na Iran linaweza kukubalika.
Inaelezwa itakuwa hivyo endapo kutakuwa na uhakikisho kwa matakwa ya Tehran kimesema chombo cha habari cha IRNA kikimnukuu mwanadiplomasia wa juu wa Iran.
Umoja wa Ulaya ulisema Jumatatu kwamba umewasilisha mapendekezo ya mwisho kufuatia mazungumzo ya siku nne ya moja kwa moja baina ya maafisa wa Marekani na Iran waliokutana Vienna.
Afisa mwandamizi wa Umoja wa Ulaya amesema hakuna mabadiliko zaidi yanayoweza kupatikana ambayo yamekuwa katika mashauriano kwa miezi 15.
Amesema anatarajia uamuzi wa mwisho kutoka pande zote ndani ya wiki chache zijazo.