Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 21, 2024 Local time: 19:31

Polisi California wawakamata wafuasi wa Trump


Mfuasi wa Trump akipambana na waandamanaji nje ya mkutano wa mgombea wa urais wa Republican, Donald Trump.
Mfuasi wa Trump akipambana na waandamanaji nje ya mkutano wa mgombea wa urais wa Republican, Donald Trump.

Watu kadhaa walikamatwa jana usiku wakati polisi walipovunja mapambano kati ya wafuasi na wapinzani wa mgombea anayewania uteuzi wa urais upande wa Republican, Donald Trump huko kusini mwa California.

Katika wakati mmoja, polisi wa kutuliza ghasia na wale waliokuwa kwenye farasi waliweka kizuizi kati ya makundi hayo mawili nje ya eneo ya Orange County kwenye Pacific Amphitheater, ambako Trump alikuwa akihutubia juu ya kampeni yake.

Madirisha ya gari la polisi yalivunjwa na watu kadhaa walijeruhiwa kabla ya mkusanyiko kuweza kudhibitiwa. Mapema jana, mgombea huyo anayeongoza alimkejeli, mgombea wa Democrat anayeongoza katika kinyang’anyiro cha kuwania urais, Hillary Clinton, akisema hatokuwa na nafasi isipokuwa kwa mtazamo wake wa kuwa mwanamke, akiwa na matumaini ya kuwa mwanamke wa kwanza rais wa Marekani.

XS
SM
MD
LG